Buja Fm

DROO YA UPANGAJI WA MAKUNDI YA MICHUANO YA AFCON U17 MWAKA 2019 KUFANYIKA KESHO MLIMANI CITY,CAF YATINGA TANZANIA.

Droo ya  upangaji wa fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa vijana wasiozidi umri wa miaka 17 (AFCON U17) zitakazofanyika Mei mwakani 2019 nchini,inatarajiwa utafanyika kesho kwenye Ukumbi wa Mlimani City mjini Dar es salaam.

Makundi hayo yanapangwa na msafara wa watu kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ambao upo nchini kwa ukaguzi kabla ya kufanyika kwa fainali mwakani.

Timu zilizofuzu kushiriki AFCON U17 Mei mwakani pamoja na wenyeji, Tanzania nyingine ni Morocco, Senegal, Guinea, Nigeria, Cameroon, Uganda na Angola.

Kwasasa wajumbe kutoka CAF wamewasili nchini Tanzania ambao ni Samson Adamu,Yasmin Hossam Eldin El Ehwany,Amri Ali Sadek,Mohamed Bakeer,Fayrouz Mahml,Mohamed Alaa El Shizy,Dina Medat,Moses Magogo anayewakilisha Kamati y Utendaji ya CAF wakati Leodger Tenga Mjumbe wa Kamati ya Utendaji CAF atakua mwenyeji wao.

Related Articles

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *